Aprili 26,2016 kumefanyika mkutano mkubwa wa wadau wa elimu wakiwemo wakuu wa shule,walimu wakuu,waratibu wa elimu kata,Chama Cha Walimua Tanzania kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga(Shinyanga Vijijini) kujadili matokeo ya mitihani ya elimu ya msingi,kidato cha pili na kidato cha nne.
Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mkutano huo mbali na kujikita katika kufanya tathmini ya matokeo hayo,pia shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani mwaka 2015 zimepataiwa zawadi ya vyeti na mbuzi huku shule zilizofanya vibaya katika mitihani hiyo zikipatiwa vyeti vya onyo na vinyago.
Mgeni rasmi katika mkutano huo Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro akatumia fursa hiyo kuwakumbusha walimu na waratibu wa elimu wa kata juu ya wajibu na majukumu yao katika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu katika wilaya,mkoa na hata taifa kwa ujumla.
Matiro aliwataka walimu kujituma kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu,kanuni na maadili ya kazi zao ikiwemo kuepuka kuwa watoro huku akiwataka waratibu wa elimu kata kuandaa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu walimu katika maeneo yao.
"Wakuu wa shule,walimu wakuu,Waratibu wa elimu fanyeni kazi vizuri,toani taarifa sahihi kuhusu walimu wenu,inashangaza kusikia shule ina walimu 11 lakini waliopo shuleni ni wawili tu,halafu wewe huna taarifa na hujui wameenda wapi,matokeo yake tunapata watumishi hewa kwa sababu ya uzembe katika kutoa taarifa sahihi",alieleza Matiro.
"Naomba kila mmoja awajibike,kuna baadhi ya wakuu wa shule hawatoi taarifa sahihi kuhusu upungufu wa madawati katika shule zao,lakini pia tumieni fedha za ruzuku zilizokuja mashuleni na waratibu wa elimu tembeleeni shule zenu badala ya kukaa tu ofisini",aliongeza Matiro.
Katika hatua nyingine aliwataka wakuu wa shule kukemea vitendo vya mimba na ndoa za utotoni na kuwaomba walimu kukaa karibu nawanafunzi wao na kuwapa elimu ya uzazi huku akiwataka kuwashughulikia wanaume wanaowapa mimba wanafunzi.
Hata hivyo alisema serikali inatambua changamoto zinazowakabili walimu na inaendelea kuzishughulikia.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kiomoni Kibamba aliwataka walimu kuwajibika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Pombe Magufuli inahitaji kila mtu afanye kazi "Hapa Kazi tu".
Mwandishi wetu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha zaidi ya 20..Angalia hapa chini
Mgeni rasmi katika mkutano huo Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa elimu katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Walimu kutoka shule mbali mbali za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo leo Jumanne,Aprili 26,2016
Mgeni rasmi Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mgeni rasmi Josephine Matiro akisisitiza jambo ukumbini
Meza kuu wakiwa ukumbini
Meza kuu
Wadau wa elimu wakiwa ukumbini
Mgeni rasmi Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Walimu wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kiomoni Kibamba akizungumza ukumbini
Wadau wa elimu wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kiomoni Kibamba akizungumza ukumbini
Viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwemo afisa elimu idara ya elimu msingi halmashauri hiyo Suzana Nyalubamba(mwenye nguo ya kijani kushoto) na afisa elimu sekondari halmashauri hiyo Stewart Makali(mwenye suti nyeusi kushoto) na mgeni rasmi wakijiandaa kutoa zawadi ya vyeti kwa shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha pili,nne na darasa la pili na la nne mwaka 2015
Zoezi la kutoa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya darasa la nne,saba,kidato cha pili na nne likaendelea
Zoezi la kutoa zawadi likaendelea
Wadau wa elimu wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Zoezi la utoaji zawadi linaendelea
Wadau wa elimu wakiwa ukumbini
Tunapokea zawadi
Zoezi la kutoa zawadi linaendelea
Zawadi la kutoa zawadi kwa shule zilizofanya vibaya nalo likawadia,wanapokea vyeti vya onyo
Napokea cheti cha onyo
Wengine walipewa zawadi ya kinyago kwa kufanya vibaya katika mitihani
Wadau wa elimu wakiwa ukumbini
Shuli zilizofanya vizuri katika somo la hisabati nazo zikapewa zawadi ya mbuzi
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin