Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha!! Maadhimisho ya Siku ya YWCA Duniani Yalivyofanyika Kanda ya Ziwa Mjini Shinyanga


Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Aprili 26,2016 kumefanyika maadhimisho ya Siku ya Chama Cha Wanawake na Wasichana( Young Women's Christian Association- YWCA) duniani ambayo kwa kanda ya Ziwa Victoria yamefanyika mkoani Shinyanga na kukutanisha wadau kutoka mikoa ya Mara,Mwanza na Shinyanga.

Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga.

Maadhimisho hayo yameanza kwa maandamano kupitia maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kisha kumalizika kwa mkutano katika viwanja vya Shycom. YWCA ni shirika lisilo la kiserikali linatoa huduma kwa wanachama na wasio wanachama bila kujali utaifa,jinsia au imani ya mtu.

Lengo la shirika hilo ni kuunganisha uongozi na sauti za wanawake na wasichana ili kujenga usawa wa kijinsia,kiuchumi,kudumisha amani na uhuru sambamba na kutunza mazingira ya ustawi wa jamii yote.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kidunia ni "Kuunda Ulimwengu Unaojumuisha Wote" huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kanda ya ziwa ikiwa ni "Kwa Pamoja Tuzuie Ndoa na Mimba za Utotoni,Tutaleta Mabadiliko Kielimu".

Washiriki wa maadhimisho hayo walisisitiza umuhimuwa jamii kuungana kwa pamoja ili kupiga vita mimba na ndoa za utotoni kwani janga kubwa sana katika kanda ya ziwa na hasa katika mkoa wa Shinyanga ambao unaongoza kitaifa kwa asilimia 59 ukifuatiwa na mkoa wa Tabora na Mara.


Akizungumza katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro alikemea tabia ya wazazi na walezi kuwapa "Samba" Watoto wa Kike "Dawa ya kusafisha nyota watoto wa kike ili wapendwe na wanaume" hali inayochangia watoto kupewa mimba wangali wadogo matokeo yake kubaki wanalalamika wakati wao ndiyo chanzo cha matatizo.


Matiro aliagiza waganga wa jadi na wazazi wanaowapa "Samba" watoto wao wakamatwe kwani wanaharibu watoto na kusababisha tatizo la mimba na ndoa za utotoni kuendelea kuwepo katika jamii.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha zifuatazo



Katibu wa YWCA mkoa wa Shinyanga Maryciana Makundi akizungumza wakati wa maadhimisho hayo katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo alisema YWCA Tanzania ilianzishwamwaka 1959 ikiwa ni miongoni mwa nchi 125 duniani zinazounganishwa na World YWCA ambayo makao yake makuu yapo Geneva Uswis.Alisema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka mwezi Aprili yakiwa na lengo la kujenga jamii yenye kuheshimu utu wa binadamu,kutetea na kulindaa haki,usawa na amani kwa wote

AKC kwaya kutoka Kanisa la Kambarage wakitoa burudani

AKC Kwaya wakitoa burudani


Kulia ni Katibu mkuu wa YWCA Tanzania Louisa Bulemela akitoa historia ya shirika hilo na jinsi linavyofanya kazi zake nchini.Alisema shirika hilo lina matawi 21 katika mikoa 11 nchini Tanzania,likiwa na wanachama zaidi ya 2000 wengi wao wakiwa ni akina mama na vijana

Wanachama wa YWCA wakiwa eneo la tukio

Tunafuatilia kinachoendelea hapa....

Maadhimisho yanaendelea


Mwenyekiti wa YWCA mkoa wa Shinyanga Neema Adam akizungumza katika maadhimisho hayo

Maadhimisho yakiendelea

Wanachama wa YWCA wakifurahia jambo
Mgeni rasmi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho hayo aliwataka wazazi na walezi kukaa na watoto wao na kuwapa elimu kuhusu afya uzazi badala ya kuona aibu
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro alipiga marufuku tabia ya wazazi kupeleka watoto wao wa kike kufanyiwa dawa za mvuto/nyota kwani vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto hao kuanza kufanya mapenzi katika umri mdogo matokeo yake wanapata mimba mimba za utotoni
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro alisema ni jukumu la kila mtu katika jamii kuwalinda watoto dhidi ya mimba za utotoni
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro pia alikemea vitendo vya kunyanyasa wajane katika jamii hasa pale wanapofiwa na waume zao kwani wamekuwa wakinyimwa haki zao ikiwemo kumiliki mali

Tunamsikiliza mgeni rasmi

Mwenyekiti wa dawati la Jinsia wilaya ya Shinyanga Pili Misungwi ambaye ni mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga akiwahamasisha akina mama,vijana na jamii kwa ujumla kutoa taarifa kwenye dawati hilo pale wanapoona watoto wanafanyia ukatili ikiwemo kupewa mimba katika umri mdogo

Misungwi alisema hivi sasa wanaendelea na zoezi la kuwakamata wasichana wanaofanya biashara ya kuuza miili yao ili kuwaepusha watoto katika jamii kuiga tabia za wanawake wanaojiuza

Mc Mama Sabuni ambye ni Muuguzi akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo alisema siku ya Jumapili wiki hii atakutana na wasichana kutoka shule mbalimbali katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini kuzungumza nao kuhusu mambo ya afya uzazi

Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea eneo la tukio

Mc Mama Sabuni akifanya yake

Mwinjilisti Esther Emmanuel akitoa neno katika maadhimisho hayo

Mwinjilisti Esther Emmanuel akiwasisitiza watoto wa kike kuacha tamaa zinazosababisha wapate mimba wangali wadogo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com