Angalia Picha- Madiwani wa Halmashauri ya Shinyanga na Kishapu Wakipewa Mafunzo ya Uongozi



Hapa ni katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo madiwani kutoka halmashauri za wilaya ya Shinyanga na Kishapu wameanza kupatiwa mafunzo ya siku nne kuhusu Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma(PS3).
 
Mafunzo hayo yamefunguliwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo kwa kuwapa maarifa na mtazamo wa pamoja juu ya usimamizi na uendeshaji wa mamlaka za serikali za mitaa,muundo wa serikali za mitaa,sheria za serikali za mitaa na masuala mtambuka katika jamii ikiwemo masuala ya Ukimwi,Jinsia na makundi maalumu-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog



Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akifungua Mafunzo hayo ambapo alisema mafunzo hayo yanafadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la Maendeleo la Marekani (USAID)yanaendeshwa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo,ambacho kina uzoefu mkubwa katika masuala ya uendeshaji wa serikali za mitaa hivyo kuwataka madiwani hao kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo hao kuwasaidia wananchi
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro akifungua mafunzo hayo



Matiro alisema mafunzo hayo pia yatalenga kuwajengea madiwani misingi thabiti katika usimamizi wa rasilimali za halmashauri na serikali za mitaa kwa ujumla sambamba na kuwajengea uwezo wa kuhoji na kusimamia mambo mbalimbali katika halmashauri kupitia vikao ikiwemo kusimamia uzingatiwaji wa taratibu za uendeshaji wa vikao katika halmashauri


Mafunzo hayo pia yatawajengea madiwani katika masuala ya usimamizi wa fedha,uibuaji wa vyanzo vya mapato na usimamizi wa manunuzi ya umma katika mamlaka za serikali za mitaa

Madiwani wakiendelea na semina hiyo ambayo inatarajiwa kuleta ufanisi katika kusimamia uendeshaji wa shughuli za serikali za mitaa

Madiwani wakiendelea na semina

Madiwani wakijadili katika vikundi kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika maeneo yao ya kazi na jinsi ya kuzitatua ili kuwaletea maendeleo wananchi

Madiwani wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post