Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa ni;
Arusha - Richard Kwitega
Geita - Selestine Muhochi Gesimba
Kagera - Armatus C. Msole
Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
Pwani - Zuberi Mhina Samataba
Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
Tanga - Eng. Zena Said
Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaa
27 Aprili, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha ndugu Albert Gabriel Msovela kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha ndugu Amantius Casmiri Msole kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha ndugu Angelina Mgeni Lutambi kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
Social Plugin