Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Vatican alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Rais Dkt. Magufuli mara baada ya kumaliza muda wake ya Ubalozi nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake nchini Francisco Montecillo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Algeria hapa nchini Belabed Saada akikabidhi ujumbe uliotoka kwa Rais wa Algeria kuja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Canada alifika Ikulu na ujumbe wake kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque wapili kutoka kulia pamoja na waakilishi wengine wa Serikali pamoja na Ubalozi wa Canada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ameikaribisha nchi ya Canada kushirikiana na serikali yake ya awamu ya
tano katika kuleta mageuzi ya kiuchumi, hususani katika uwekezaji kwenye
sekta ya Kilimo, Madini, Uvuvi na Huduma za kijamii.
Rais
Magufuli ametoa ujumbe huo alipokuwa akizungumza na Balozi wa Canada
hapa nchini Mheshimiwa Alexandre Le've'que aliyekutana nae Ikulu Jijini
Dar es salaam na kupokea barua yenye ujumbe wa Waziri Mkuu wa Canada
Mheshimiwa Justin Trudeau.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Magufuli amesema serikali yake hairidhishwi na
jinsi kilimo cha Tanzania kisivyowanufaisha wakulima ipasavyo, na hivyo
ameikaribisha nchi ya Canada hususani sekta binafsi ya nchi hiyo
kushirikiana na Tanzania kujenga viwanda vya kusindika mazao ya kilimo
na uvuvi ili kuzalisha ajira na kuongeza thamani ya mazao kwa manufaa ya
wananchi wa nchi zote mbili.
Dkt.
Magufuli pia ametaka Canada yenye uwezo mkubwa kiteknolojia na mtaji
ishirikiane na Tanzania katika uwekezaji kwenye sekta ya madini na gesi
kwa kujenga viwanda vya kuchakata madini ndani ya nchi ya Tanzania na
pia rasilimali ya gesi ambayo mpaka sasa Tanzania imethibitika kuwa na
hifadhi ya futi za ujazo zaidi ya Trilioni 57.
"Mheshimiwa
Balozi Alexandre Le've'que naomba ukamweleze Waziri Mkuu wa Canada
Mheshimiwa Justin Trudeau kuwa Tanzania na Canada sio tu ni nchi
marafiki bali pia ni ndugu wenye uhusiano wa kihistoria. Ningependa
kuona Canada inashirikiana na serikali yangu, katika juhudi zake za
kuachana na usafirishaji wa mchanga wa madini badala ya madini
yaliyochakatwa na pia kuachana na usafirishaji wa mazao yakiwa ghafi" Amesema Rais Magufuli.
Kwa
upande wake Balozi wa Canada hapa nchini Mheshimiwa Alexandre Le've'que
amemhakikishia Rais Magufuli kuwa atafikisha ujumbe huo kwa Waziri Mkuu
Canada Mheshimiwa Justin Trudeau, na amebainisha kuwa nchi hiyo ipo
tayari kushirikiana na Tanzania katika juhudi zake za kuimarisha uchumi,
hasa baada ya kujionea juhudi za Rais Magufuli katika kukabiliana na
rushwa, kuongeza ukusanyaji wa mapato na kusimamia nidhamu ya kazi kwa
watumishi wa umma.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amepokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Aljeria
Mheshimiwa Abdelaziz Bouteflika ambaye pamoja na kumpongeza kwa hatua
anazochukua katika uendeshaji wa serikali, amemhakikishia kuwa Aljeria
ipo tayari kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo kati yake na
Tanzania huku akitaja maeneo ya kipaumbele kuwa ni nishati na kilimo.
Ujumbe
wa Rais Bouteflika umewasilishwa kwa Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es
salaam na Balozi wa Aljeria hapa nchini Mheshimiwa Belabed Saada.
Rais
Magufuli amemhakikishia Rais Bouteflika kuwa Serikali yake itaendeleza
na kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Aljeria, na kwamba hivi
karibuni imepanga kuanzisha ofisi za Ubalozi katika nchi hiyo.
Kuhusu
sekta za nishati na kilimo, Rais Magufuli amesema serikali yake
inakaribisha uwekezaji kutoka Aljeria hasa wakati huu ambapo Tanzania
imethibitika kuwa na kiasi kikubwa cha gesi, na kwa upande wa kilimo
ametoa wito kwa Aljeria kushirikiana na Tanzania katika mpango wake wa
kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, ikiwemo usindikaji wa
zabibu, viwanda vya nguo, viwanda vya ngozi na nyama na viwanda vya
kusindika minofu ya samaki.
"Naomba
ukamweleze Mheshimiwa Rais Bouteflika kuwa Tanzania itaendeleza na
kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Aljeria na kwamba imefurahishwa
sana kuona Aljeria ipo tayari kusaidia juhudi za kuendeleza sekta ya
kilimo nchini Tanzania" Rais Magufuli amemweleza Balozi Belabed Saada.
Katika
hatua nyingine, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Balozi wa
Vatican hapa nchini Mheshimiwa Francisco Montecillo ambaye anamaliza
muda wake baada ya kuiwakilisha Vatican kwa muda wa miaka minne na nusu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
22 Aprili, 2016