Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Dereva Tax Afa Maji Baada ya Kusombwa na Maji Akivuka Mto na Gari Lake

Dereva tax aliyejulikana kwa majina ya Shakiru Hashimu mkazi wa Mdaula Ngerengere mkoani Morogoro amekufa maji baada ya kusombwa akiwa ndani ya gari wakati akijaribu kuvuka mto Ngerengere.

Dereva huyo alikuwa akivuka mto huo ukiwa umefurika maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.

Mwandishi wa habri hizi amefika katika eneo la tukio na kukuta kikosi cha jeshi kikifanya uokozi wa kuopoa mwili na gari lililo zama katika mto ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiomba serikali kuweka kingo za vyuma pembeni mwa daraja hilo ili kuzuia ajali za kutumbukia magari.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tukio hilo ni la kusikitisha ambapo amewatahadharisha wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini wakati wanapovuka mito kutokana na mito mingi kujaa maji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com