Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Fastjet Yashinda Kwenye Tuzo Za Usafiri Duniani













TAARIFA KWA NYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam – 11 April 2016 
 
Fastjet, shirika la ndege la gharama nafuu barani Afrika limeshinda Tuzo ya Shirika la Ndege Linaloongoza Afrika kwa gharama nafuu kwenye Tuzo ya 23 ya Mwaka ya Usafiri Duniani iliyotolewa Zanzibar, Tanzania Aprili 9, 2016.

Tuzo ya Usafiri ambayo inatambulika duniani imepangwa kwa kutambua, kutuza na kusherehekea mafanikio kwenye sekta zote muhimu za usafirishaji wa kwenye sekta ya utalii.


Tuzo ya Shirika la Ndege Linaloongoza kwa Gharama Nafuu ambayo hutolewa kwa wataalamu wa usafiri na utalii pamoja an watumiaji duniani kote inatokana na kutambua huduma za fastjet za kufanya watu wamuumudu usafiri wa anga, usalama na kuaminika kwenye mtandao yote barani Afrika.



“Kutambuliwa na kupata tuzo hii sio tu kunaonesha kujituma kwa ufanisi kwenye usafiri wa anga, lakini kunaonesha matokeo ya juhudi zetu tunazojaribu kulifanyia bara la Afrika,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse na kuongeza, “tunajivunia sana kupokea kutambuliwa huko na sekta hii kubwa na fastjet itaendelea kuufanya usafiri wa anga kuwa wa gharama za chini ambazo watu wengi watazimudu barani Afrika.”



Shirika hilo la ndege la bei nafuu lilizinduliwa Novemba 2012 na linafanya safari kadhaa za ndani ya Tanzania kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya, Mwanza na Kilimanjaro. Kukua kwa mtandao wa fastjet pia kunatoa huduma kwa njia ya kutoka Dar es Salaam na Zanzibar na kwenye vituo vya kimataifa kama vile Johannesburg, Harare, Victoria falls, Entebbe, Nairobi na Lusaka.



Fastjet inatarajia abiria wake wengi kwenye njia hizo inakotoa huduma kuwa ndio wanasafiri kwa mara ya kwanza kwa kutumia ndege kutokana na sababu ya kukwazwa na tozo za nauli ya juu ambazo awali hawakumudu kulipa kwa ajili ya usafiri huo.



Huduma hii ya nauli nafuu imeungwa mkono kwenye utafiti uliofanywa na shirika hilo hivi karibuni, unaoonesha kuwa asilimia 40 ya abiria kwenye njia zote walikuwa ndio mara yao ya kwanza kusafiri kiumudu kusafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza hivyo pongezi ziende kwa gharama nafuu za fastjet.



Jambo jingine ambalo linapatikana kwenye njia inamopita fastjet ni kuboreshwa kwa mbadala wa mzigo ambako kunajulikana kama ‘freighty’ kunakoruhusu abiria kusafirisha hadi kilo 80 zilizofungwa kwenye mabegi kwa gharama ya shillingi 88,000. Mbadala huo wa kusafirisha mizigo kimsingi umekuwa ni maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na fastjet kwenda kununua bidhaa za jumla kimataifa na kuzisafirisha kwa ajili ya kuziuza kwenye masoko ya nyumbani mwao.




Tuzo hii inaongeza idadi ya tuzo ambazo fastjet imeshazipata zikiwemo kushinda Tuzo ya Ubunifu kwenye Usafiri kwenye utoaji wa nane wa tuzo hiyo mwaka 2015, na hali kadhalika kutangazwa kuwa shirika la ghama nafuu barani Afrika katika kulinganishwa mengine kwenye usafiri wa anga kupitia mtandao wa safiri WhichAirline.com in 2016.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com