Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imempa dhamana Mtuhumiwa Isaac Abakuki anayetuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Hakimu mfawidhi Agustino Rwezire amesema Mahakama baada ya kupitia hoja mbili zilizotolewa na upande wa mashtaka na mshtakiwa, imeridhia kutoa dhamana kama haki ya msingi ya mshtakiwa kutokana na kosa alilotenda ambapo dhamana hiyo ni ya Wadhamini wawili waliotakiwa kuwa na jumla ya shilingi milioni tano.
Kwenye siku ya kwanza kufikishwa Mahakamani Polisi walisema Tarehe 17 March 2016 Isaac Abakuki akiwa nyumbani kwake Olasiti Arusha alipokea ujumbe kwenye account yake ya Facebook ukisema ‘mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere’ ukiwa ni Ujumbe wa mjadala ulioanzishwa kwenye mtandao wa kijamii kufuatia hatua ya Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 CloudsTV na kuwapongeza Watangazaji wa kipindi hicho.
Baada ya kusoma huo ujumbe Mtuhumiwa aliandika comment kujibu alichokisoma na kuandika ; ‘Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana“….. comment ya mtuhumiwa iliwaudhi na kuwakwaza watu wengi walioona Facebook na wakaamua kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA.
TCRA kwa kushirikiana na Polisi baada ya kufanya uchunguzi wa kina walifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa 22 March 2016 kwenye hoteli ya Annex Arusha na alipandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza April 15 2016, kesi yake itaendelea tena May 17 2016.
Social Plugin