Abiria nane na marubani wawili waliokuwa kwenye ndege ya kampuni ya AURIC iliyokuwa ikitokea jijini Mwanza wamenusurika kifo baada ya ndege hiyo kupasuka tairi la mbele na kupoteza mwelekeo wakati ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.
Akizungumzia tukio hilo meneja wa uwanja wa ndege wa
Bukoba, Doris Uagile amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya asubuhi
na kwamba ndege hiyo ilipopasuka tairi ilikosa mwelekeo na kuelekea
kwenye majani yaliyoko pembeni mwa uwanja huo.
Amesema katika
tukio hilo kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa na abiria waliokuwa wasafiri
na ndege hiyo kutokea Bukoba kuelekea Mwanza walitafutiwa usafiri
mwingine.
Nao baadhi ya wananchi katika manispaa ya Bukoba walioshuhudia
tukio hilo wamesema walisikia kishindo kikubwa na baadae wakaona ndege
ikiingia kwenye majani.
Social Plugin