Rais John Magufuli ameahirisha shamrashamra za kikukuu ya kumbukumbu ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo hufanyika kila mwaka, Aprili 26.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Rais Magufuli amewataka wananchi kusherehekea siku hiyo kwa kupumzika majumbani kwao na katika shughuli zao binafsi.
Aidha, fedha zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya kugharamia vyakula, vinywaji, gwaride na mengineyo ameagiza zielekezwe katika upanuzi wa barabara ya Mwanza ‘Mwanza – Airport’, katika eneo linaloanzia Ghana Quarter hadi katika uwanja wa ndege jijini humo, kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.
Hii ni Taarifa Rasmi kutoka Ikulu
Social Plugin