Aliyekuwa mchezaji miereka na nyota wa filamu za ngono Chyna amefariki akiwa na umri wa miaka 45.
Meneja wake amethibitisha habari hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter.
''Ni masikitiko makubwa kutangaza kwamba tumempoteza shujaa'',ulisema ujumbe huo,akiongezea kuwa:Ataishi kukumbukwa na mashabiki wake wengi na sisi sote tuliompenda.
Chyna alipatikana amefariki nyumbani kwake katika ufukwe wa bahari wa Redondo,mjini California,baada ya kurudi nyumbani kutoka Japan.
Chyna alipochumbiwa na mchezaji mwenza wa miereka
Mapema wiki hii alichapisha kanda ya video yenye urefu wa dakika 13 ambapo anazungumza kuhusu kuanzisha biashara mpya ya chakula.
Alionekana akikosea baadhi ya maneno aliyokuwa akiyatamka na anaonekana amechanganyikiwa.
Alijitahidi kukabiliana na dawa za kulevya wakati wote wa kazi yake na alionekana katika kituo cha kuwarekebisha tabia watu maarufu mwaka 2008.
Via>>BBC
Social Plugin