Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mfanyabiashara Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Gesti



Mfanyabiashara wa mazao, Eliusta Peter(40), amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika nyumba ya kulala wageni wilayani Kilombero.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea Aprili 22 baada ya wahudumu wa nyumba ya wageni ya Sayari kubaini maiti katika chumba namba mbili.


Inadawa Aprili 20 mwanamke huyo akiwa na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na kuchukua chumba kimoja wakisema wao ni wafanyabiashara wa mazao.

“Mwili wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayari chumba namba mbili saa 11 jioni na ulipochunguzwa ikagundulika kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya jereha,”alisema Matei.


Mwanamke huyo alikuwa na jeraha kushoto mwa bega lake lililotokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali


Matei alisema kwa taarifa walizozipata bila shaka kijana aliyekuwa naye anahusika na mauaji hayo.


Wakati huo huo, jeshi la polisi wilayani Kilosa limemkamata Rogasian Jeremia kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Faustina Sizayi(25) kwa kumkatataka kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.


Mtuhumiwa alikamatwa akiwa anajihusisha na kazi ya ulinzi wa maduka baada ya polisi kumsaka kwa muda mrefu na ndipo Aprili 24 alikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com