Watanzania waishio Marekani juzi waliamka na habari zilizowashitua kuhusu kuuawa kwa mwenzao katika jiji la Houston Texas Marekani aitwae Henry Kiherile ambapo Polisi Marekani inaendelea kulichunguza tukio.
Kitengo cha upelelezi wa mauaji idara ya Polisi Houston Texas kimesema kwamba Henry aliuwawa kwenye tukio lililohusisha wizi wa gari lake aina ya BMW na mpaka sasa Polisi hawajui sababu hasa za tukio hilo na ilianzaje lakini bado upelelezi unaendelea.
Dr. Leonard Tenende ambaye ni Mume wa mama mkubwa wa Marehemu ambao ndio walimpokea Henry na kuishi nae kwenye siku za mwanzoni Marekani, amesema ‘Polisi wameanza kufatilia mwenendo wa Marehemu kuanzia siku ilipoanza na mpaka sasa hawajalipata gari na bado hawajatueleza au kutupa taarifa za ziada‘
Houston Texas
Dr. Tenende amesema jambo lililowazi ni kuwa Marehemu aliingiliwa katika gari lake na hilo linaleta maswali zaidi kuhusu dakika za mwisho za uhai wake ila kifo hakikutokea nyumbani kwake au mtaani kwake, Polisi wanasema walipata taarifa toka kwa dereva aliyepita kwenye eneo la tukio saa sita na robo usiku kwamba kuna mtu mwenye majeraha, kikosi cha zimamoto kikafika eneo la tukio na kumchukua mpaka Hospitali.
Kwa mujibu wa Majirani kwenye eneo la tukio ni kwamba milioni ya risasi ilisikika kisha gari kuondoka kwa kasi ambapo Dr. Tenende anasema ‘ilichukua muda Marehemu kusaidiwa na kabla ya simu kupigwa Polisi kuomba msaada bado alikua hai, labda taarifa zingefika mapema zaidi asingefariki maana amefia kwenye gari la Wagonjwa akipelekwa Hospitali‘
Henry Kiherile alikua na umri wa miaka 32 na alisifiwa kwa kuonyesha uwezo mkubwa kwenye masomo Marekani na alikua amemaliza Degree yake kwenye mambo ya Accounting na alikua anajiandaa kwa mitihani kujiunga na shule ya Sheria, weekend hii Watanzania Marekani wanamuaga kabla ya kusafirishwa kuja kuzikwa Tanzania.
Polisi wa Houston Texas wameahidi wiki ijayo kuwasiliana na ripota wa millardayo.com Marekani Mubelwa Bandio ili kutoa taarifa zaidi kutoka kwenye ofisi inayoshughulikia file la mauaji ya Henry.
Social Plugin