Katika mataifa mengi ya Afrika wakati wa uchaguzi wanasiasa hutoa pesa ilikuwashawishi wapigaji kura kuwachagua.
Lakini huko Korea Kusini amini usiamini, polisi wameanzisha uchunguzi baada ya kuibuka madai kuwa wapiga kura wenye umri wa makamo walimpigia mwanasiasa fulani eti kwa sababu aliwapa vidonge vya kuongeza nguvu za kiume!
Yamkini mwanasiasa mmoja aliwashawishi watu hao wenye umri wa makamo kwa kuwapa vidonge.
Mbunge wa eneo hilo la Suwon iliyoko karibu na mji mkuu wa Seoul ndiye anayetuhumiwa kwa njama hiyo.
Suwon ilishuhudia upinzani mkali katika uchaguzi uliofanyika Jumatano iliyopita.
Jina la mshukiwa mkuu halijatajwa hadi ushahidi utakapopatikana.
Hata hivyo uchunguzi wa msingi umethibitisha kuwa mgombea huyo alikuwa na kiwango kikubwa mno cha madawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa wakati mmoja.
Haijabainika ni kwanini wala alikusudia kuwapa kina nani.
Uchunguzi bado unaendelea.
Via>>BBC
Social Plugin