Habari
hiyo imeandikwa kufuatia ufafanuzi uliotolewa na Bunge jana kuhusu
maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) dhidi ya
utekelezaji wa mkataba wa Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi
Enterprises Ltd kuhusu mradi wa utambuzi wa alama za vidole (AFIS)
(Automated Fingerprint Identification System.)
Ndani
ya habari hiyo pia, Gazeti hilo limeeleza kuwa kamati ya PAC iliwahi
kuliandikia Jeshi la Polisi kulitaka liwasilishe mkataba huo mbele ya
Kamati, jambo ambalo si kweli bali ni upotoshwaji wa makusudi wenye
lengo la kujenga hisia mbaya kuhusu mwenendo wa shughuli za Bunge mbele
ya Umma.
Ukweli
ni kwamba PAC haijawahi kuliandikia jeshi la Polisi kama inavyodaiwa na
Gazeti hilo. Nukuu ya maelezo ya PAC katika Hansard kwa Afisa Masuhuli
kuhusu jambo hilo inasema kama ifuatavyo:
“Kamati
inamuagiza Afisa Masuhuli kuwasilisha maelezo ya kina kuhusu
utekelezaji wa Mkataba baina ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi
Enterprises kuhusu mradi wa AFIS. Maelezo hayo yawasilishwe kwa Ofisi
ya Katibu wa Bunge kabla ya Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2016”.
Katika
agizo hilo PAC haikuwa imeandika kwa maandishi kuhusu agizo lake hilo
hadi tarehe 12 Aprili, 2016 ilipo mweleza Katibu wa Bunge aweze
kuwasilisha agizo hilo kwa maandishi ili liweze kupata Kinga chini ya
Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ambapo barua iliandikwa na
kuwasilishwa kwa Afisa Masuhuli ili kupatiwa maelezo hayo kabla ya
tarehe 18 Aprili, 2016.
Aidha,
Mwandishi pia amelituhumu Bunge kuwa lina nia ya kuficha ukweli kuhusu
jambo hili kwa kusema taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa na Bunge ni “kama
kufunika kombe mwanaharamu apite kwa kujaribu kupotosha maagizo ya
yaliyotolewa na kamati ya PAC ambayo inataka kuuona mkataba huo”
Ni
vyema ikafahamika kuwa si jambo jema kwa mwandishi au chombo chochote
cha habari kulituhumu Bunge linapotekeleza majukumu yake kwa kuwa Bunge
linafanya kazi zake kwa kwa kuzingatia kanuni zake za Kudumu ikiwa ni
pamoja na Sheria.
Ofisi
ya Bunge inalisihi Gazeti la Nipashe kuomba radhi kutokana na taarifa
yake hiyo iliyojaa upotoshwaji mkubwa kwa uzito ule ule au kurekebisha
taarifa yake kulingana na ukweli ulivyo haraka iwezekanavyo.
Imetolewa na;
Ofisi ya Bunge,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM.
16 Aprili, 216.
Social Plugin