Rais
wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua
mwenyekiti wa chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed kuwa mjumbe wa Baraza
la wawakilishi.
Uteuzi
huo wa Rais Dkt Shein umefuata baada ya leo kutoa hotuba na kuzindua
Baraza la wawakilishi ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umoja
na mshikamano miongoni mwa wananchi.
Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na
1.Mohamed aboud Mohamed
2. Amina Salum Ali
3. Moulin Castico
4. Balozi Ali karume
5. Said Soud Said na
6. Juma Ali Khatibu
Aidha uteuzi huo umeanza hii leo tarehe 05.04.2016.
Social Plugin