Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TCRA :Asilimia 18 Ya Simu Za Kiganjani Ni Bandia ,Asilimia 79 Ndiyo Ziko Salama


MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha Desemba hadi Februari mwaka huu ziko salama na sio za bandia ,huku asilimia 18 zikionekana zikiwa za bandia hivyo kuwataka wananchi kutambua kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache tofauti na kipindi cha nyuma.


Pia imebainika kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua na umeme ni kutokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa kuhimili mionzi pindi zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha mlipuko wa moto na hivyo kuleta madhara .


Hayo yalisemwa na meneja uhusiano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Innocent Mungi alipokuwa akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani iliyowashirikisha wadau na wafanyabiashara wa jijini hapa.


Alisema kuwa kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina matatizo ya aina yeyote.


Alidai kuwa kufuatia uzimaji wa simu bandia litakalofanyika juni 16 mamlaka hiyo imeweza kutoa elimu kwa wauzaji,watumiaji ili kuhakikisha kuwa wanabini simu zao kama ni salama ili kuweza kuepuka zoezi la kuzimiwa simu zao bila yawao kujiandaa.


“Wakati tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa asilimia 30 zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February simu bandia zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache mno “aliongeza .


Aidha Innocent alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kupunguza wizi wa simu na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitumika mara nyingi kwa njia ya simu hizo pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.


Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Ally Simba aliwataka wananchi kufanya zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo juni 16 ,kwani wengi wa watumiaji wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia .


Simba aliseama kuwa ni vema wananchi wakatumia mfumo waliowekewa wa kubaini simu zao kama ziko salama kwani ifikapo juni simu zote bandia zitazimwa na kuwataka wafanyabiashara nao wawe makini pindi wanaponunua mizigo yao ya bashara ili kuepuka hasara watakazozipata wao na pia hasara watakazopata wanunuzi wa simu hizo .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com