Wanawake wawili vikongwe wameuawa kinyama kwa kupigwa na kukatwa katwa kwa mapanga kisha miili yao kuchomwa moto katika kijiji cha Kenyamsana wilayani Rorya mkoani Mara kwa tuhuma za kujihusisha na ushirikina.
Tukio hilo limesababisha hofu kubwa kwa wanawake wengi wenye umri mkubwa katika kijiji hicho.
Wakizungumzia tukio hilo la kwanza kutokea wilayan Rorya, baadhi ya ndugu wa marehemu hao, wamesema kuwa kundi la watu waliwakamata wanawake hao vikongwe kisha kuwapiga katika sehemu mbalimbali za miili huku wakiwaingiza kwa nguvu ndani ya nyumba zao ambazo zimeezekwa kwa kutumia nyasi na kuwachoma moto.
Kufutia tukio hilo la kusikitisha na la kikatili Mwenyekitiwa kamati ya ulinzina usalma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Rorya Bw Felix Lyaniva, amefika eneo la tukio na kuliagiza jeshi la polisi kuwakata watu wote ambao wamehusika kufanya kitendo hicho cha kinyama kwa kuanzia na viongozi wa vitongoji katika eneo hilo.
Tayari Jeshi la Polisi limewakamata watu 13 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ya wanawake hao vikongwe Bi Ghati Ndege na Nyakorema Waryuba wote wakazi wa k ijiji hicho cha Kenyamsana wilayani Rorya.
Social Plugin