Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Rabi Hume wa Modewjiblog)
Wananchi wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia nafasi za kufanya baishara zilizopo kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo makubaliano ambayo yanawapa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara kwa uhuru.
Hayo yamesema na Mbuge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na kusema kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho wa kisiasa.
Amesema kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya baishara katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya kusambaza bishaa zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Huu ni muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya baishara kwa nchi za Afrika Mashariki, vikwazo zilivyopo kwa sasa ni wananchi wengi wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo lakini tumejipanga katika hilo,” amesema Nyerere.
Amesema kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na ushirikiano huo.
Amesema programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu, vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la Feri.
Pia Nyerere amewataka Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa mbalimbali kupitia mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na fursa nyingi ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.
Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza jambo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakichukua habari.
Social Plugin