Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Watu 40 Wanusurika Kifo Ajali ya Gari Jijini Mwanza,15 Wajeruhiwa Vibaya



Zaidi ya watu 40 wamenusulika kifo kati yao 15 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka katikati ya jiji la Mwanza kwenda Igombe kuacha njia na kutumbukia kwenye mtaro wa barabara ya Pasiansi Airpoti eneo la Iloganzala hali iliyosababisha msongamano wa magari katikati ya jiji. 
 
 
Aliyekatika mkono kutokana na ajali ya gari la abiria namba T 764 AMD aina ya Isuzu huku baadhi ya majeruhi waliofikishwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure wakibainisha chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi. 
 
 

Akithibitisha kupokea majeruhi 12 afisa muuguzi katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure Bi.Leya Mwalongo amesema kuwa kati ya majeruhi 12 mmoja hali yake siyo nzuri atahamishiwa hospitali ya rufaa Bugando. 
 
 

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza ACP Japhet Lusingu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha majeruhi 15 ambapo dereva wa gari hilo ametoroka na kwamba juhudi za kumtafuta zinaendelea. 
 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com