Watu Wanane Wafariki Kwa Mafuriko Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro



Zaidi ya kaya 2200 katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro hazina mahala pa kuishi, wala chakula na mahitaji mengine muhimu ya kibinadamu, kufuataia mvua kubwa zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo na kusababisha maafa makubwa ya vifo,mali na mashamba. 
 
 
Wananchi wa kijiji cha soko kata ya Kahe mashariki ambao bado maeneo yao yamezingirwa na maji wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwapa msaada wa haraka wa chakula na dawa za binadamu kwa ajili ya kujikinga na magonjwa ya milipuko na njaa. 
 

Wamesema mvua hizo zimesababisha madhara ya vifo vya mifugo, mazao ya chakula kungolewa na maji,samani za ndani kwenda na maji na nyumba kadhaa kuanguka huku vijiji vitano vya Kahe mashariki na Kahe magharibi vikiwa vimezingirwa na maji. 
 

Kutokana na madhara hayo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw.Saidi Meck Sadic ameamuru shamba la mwekezaji wa Soko estate lenye ukubwa wa ekari 3000 ambalo halijaendelezwa kwa zaidi ya miaka 40, ligawanye kwa wahanga wa mafuriko hayo. 
 

Mafuriko hayo ya Aprili 23 na 24, yamegharimu maisha ya watu wanane hadi kufikia sasa,huku mamia ya wakazi wa kata mbili za Kahe magharibi na Kahe mashariki zikiwa bado zimezingirwa na maji.
 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post