Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Awasili Dar Kwa Kishindo Akitokea Uganda


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwasili jijini Dar es salaam jioni hii, akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo.



Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka Jijini Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini Kampala. Mbali na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio walipokuwa wakimsubiria Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alierejea jijini Dar es salaam leo akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga.

Tazama Video hapa chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com