Jumamosi Mei 07,2016 Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella(pichani),ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mwanza amefanya kikao na watendaji wa serikali ngazi ya wilaya na mkoa kilicholenga kutoa maelekezo mbalimbali ya kiutendaji ikiwa ni siku chache tu baada ya kupewa majukumu na rais John Pombe Magufuli ya kuusimamia mkoa wa Shinyanga ambao sasa hauna mkuu wa mkoa baada ya rais kutengua uteuzi aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Anne Kilango Malecela kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu watumishi hewa mkoani humo.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Shinyanga,Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde anaripoti
Akizungumza katika kikao hicho Mongella aliwataka watendaji wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea na ubabaishaji ili kuepuka kutumbuliwa majipu kwani serikali ya awamu ya tano inataka kila mtu kuwajibika kwa nafasi yake.
Mongella aliwasisitiza kutafuata miongozo ya kazi na kuacha masuala ya uzembe na ubabaishaji kazini kwa kuwajibika ipasavyo bila ya kusubiri kusukumwa, hataguswa na suala la kutumbuliwa majipu na atafanya kazi yake kwa amani bila hofu yoyote.
“Usisubiri kusukumwa ndiyo ufanye kazi, kama kuna mtendaji wa serikali ambaye mpaka sasa hajajua serikali hii inataka nini,basi akae pembeni ukitaka kufanya kazi kwa amani, bila ya hofu yoyote fuata sheria,miongozo na taratibu za serikali na hakuna mtu atakayekugusa kukutumbua jipu”,alisema Mongella.
Mongella alizitaka halmashauri zote sita za mkoa huo kusimamia kikamilifu shughuli za maendeleo na kudhibiti ubadhilifu wa fedha katika halmashauri hizo.
Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kukamilisha masuala ya utengenezaji wa madawati katika shule na kutangaza kuwa mpaka kufikia tarehe Juni 30 mwaka huu kusiwe na upungufu wa madawati katika kila shule mkoani humo na atakayeshindwa kutimiza agizo hilo ajiandae kuwajibishwa.
“Hili ni agizo la mheshimiwa rais,ifikapo Juni 30,2016 kusiwe na tatizo la madawati shuleni,wapo baadhi ya watendaji wanafikiri ni utani,hapa hakuna siasa ni kazi tu,wengine wanaandaa taarifa za kujitetea za kushindwa kumaliza changamoto ya madawati,Timiza wajibu wako kwa wakati,usitayarishe maelezo yatakuponza tarehe 1,Juni mwaka huu kila mkurugenzi afanye uhakiki wa madawati katika shule zake”,alisema Mongella.
Angalia picha 24 wakati wa kikao hicho......
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifungua kikao hicho Aliyesimama ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella akizungumza katika kikao hicho,kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,kulia ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela
Wajumbe wa kikao hicho wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri za wilaya,wakuu wa wilaya,wakuu wa idara,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa,waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wa serikali ngazi ya wilaya na mkoa wakiwa ukumbini
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella akizungumza ukumbini ambapo alisema bado hajaridhika na idadi ya watumishi hewa mkoani Shinyanga hivyo atahakikisha kwa kushirikiana na katibu tawala na kamati ya ulinzi na usalama mkoa kuwa watumishi hewa wengi zaidi wanaibuliwa
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa (kushoto) na mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'humbi ( kulia) wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza katika kikao ambapo alimhakikishia kaimu huyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella kuwa atajitahidi kusimamia maagizo hayo yote ikiwamo ya ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akiwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Alhaj Kusilawe wakiwa meza kuu
Tunafuatilia kinachoendelea humu.....
Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea...
Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr.Ntuli Kapologwe(kulia) akiwa ukumbini
Akitoa neno la shukrani mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(pichani) alimuomba mkuu huyo wa mkoa kuwasaidia kazi za mkoa wa Shinyanga kwani mkoa huo haukuwa na mlezi kwa muda mrefu na sasa mkoa utapiga hatua kubwa kimaendeleo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin