Watu wasiojulikana wakiwa na pikipiki aina ya Boxer,usiku wa kuamkia leo wamemuua kwa kumpiga risasi kadhaa katika sehemu mbalimbali za mwili wake askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani, Ally Kinyogoli nyumbani kwake Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.
Baada ya kumuua, watu hao walitokomea kusikojulikana bila kuchukua kitu chochote.
Kinyogoli alijizolea umaarufu katika kipindi cha redio One kila siku asubuhi alipokuwa akitoa taarifa za hali za barabarani zikiwemo njia zenye foleni kwa wakazi wa jijini.
Social Plugin