Mchekeshaji
maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show, Mohammed
Abdallah ‘Kinyambe’ amefariki dunia leo Jumatano baada ya kusumbuliwa
kwa muda mrefu na uvimbe tumboni.
Taarifa
za kifo chake zimeanza kusambaa usiku huu katika mitandao ya kijamii baada
ya wasanii wa filamu kuanza kupost picha mbalimbali huku wakiandika RIP
Kinyambe.
Mmoja
kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania,
Mkono Mkonole, amesema Kinyambe amefariki usiku akiwa mkoani Mbeya.
“Kinyambe
alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni kwa muda mrefu, ila leo ndiyo
amefariki akiwa mkoani Mbeya, katika hospitali ya mkoa wa Mbeya,” alisema Mkonole.
Kuhusu taratibu za mazishi, Mkonole amesema bado hawajapanga kwani taarifa za kifo chake wamezipokea usiku.
“Kusema
kweli bado hatujapanga kuhusu mazishi, lakini sasa hivi tunawasiliana
na ndugu zake ili kujua taratibu za mazishi na zikikamilika tutaweka
wazi,” alisema Mkono.
Kinyambe atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuigiza, hasa hasa jinsi anavyoongea pamoja na mtindo wake wa pekee wa kugeuza macho..
Mungu amlaze mahali mahali pema peponi -Amina
Hizi Hapa ni baadhi ya picha zake...baada ya picha nimekuwekea Video 5 za Kinyambe enzi za uhai wake akifanya vituko vyake
Social Plugin