Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Haya Ndiyo Maamuzi ya Mahakama Kuu Tabora Kwenye Kesi ya Ubunge ya Kafulila

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora iliyokuwa inasikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila imetoa hukumu ambapo David Kafulila ameshindwa kwenye kesi hiyo dhidi ya Mbunge Kigoma kusini, Hasna Mwilima ‘CCM’.


Kesi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora na ilikuwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.

Katika kesi hii upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kennedy Fungamtama pamoja na Mawakili wa Serikali upande wa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com