Uzinduzi wa basi la wanawake pekee katika mji mmoja wa China umewakasirisha wanaume wa taifa hilo na kuzua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii.
Huduma hiyo mpya itatolewa wakati wa asubuhi na wakati wa shughuli nyingi katika mji wa mashariki wa Zhengzhou katika juhudi za kupunguza visa vya wanawake kusumbuliwa na wanaume kulingana na gazeti la Dahe daily.
Kampuni hiyo ya basi itawalinda wanawake dhidi ya kunyanyaswa wakati wanapovaa nguo nyepesi huku wanawake wanaonyonyesha wakihisi wapo salama.
Treni za wanawake na mabasi yameanzishwa katika mataifa mengi na kuonyesha ufanisi mkubwa, lakini magari ya uchukuzi ya watu wa jinsia moja ni swala jipya nchini Uchina.
Wanawake waliohojiwa ndani ya basi hilo wanasema wanafurahishwa na huduma hiyo huku mmoja akimwambia ripota kwamba ni heshima kubwa kwa wanawake.
Lakini baadhi ya wanaume hawafurahii jambo hilo.
Mmoja aliliambia gazeti la Dahe Daily kwamba unyanyasaji sio jambo la kawaida katika magari ya uchukuzi.
Kampuni ya basi hilo imewakejli wanaume ikisema:Hatua hii itawafedhehesha wanaume.
Mtu mwengine amelalamika katika kituo cha redio cha Uchina:Nililazimika kungojea sana kwa basi jingine kuwasili kwa kuwa sikuruhusiwa ndani.
Social Plugin