Lady Jaydee Amtaka Gardner Aombe Radhi Ndani ya Siku 7 ..Kauli ya “Nimeshamkojoza Kwa Miaka Kama 15 Hivi”


Msanii wa muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kupitia mwanasheria wake Aman G. Tenga kutoka Law Associates (Advocate) ameandika barua ya kumtaka mtangazaji maarufu wa Clouds Fm, Gardner G. Habash, kuomba msamaha mbele ya umma kutokana na kauli yake ya uzalilishaji aliyoitoa dhidi yake.



Gardner ambaye alikuwa mume wa muimbaji huyo wa Ndindindi, anatuhumiwa kulifanya kosa hilo mnamo tarehe 6 May 2016, akiwa kama mshereheshaji tamasha la Miss TIA 2016 lililofanyika CDS Park (zamani TCC) ambapo alidaiwa kutamka kwa makusudi maneno ya udhalilishaji na kejeli “Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi” mbele ya umma. 



Baada ya wiki moja toka tukio hilo kutokea, Lady Jaydee kupitia mwanasheria wake ameandika barua hii.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post