Zaidi ya mabasi 34 katika mradi wa mabasi yanayoenda haraka yamepata ajali kwa kipindi cha siku 20 toka kuanza rasmi mradi huo kutokana na baadhi ya wananchi na madereva wa magari ya kawaida kutumia barabara maalum za mradi wa DART.
Takwimu hizo zimetolewa na meneja uhusiano wa mabasi yao -UDART- Bwana Deus Gugaiwa baada ya kuibuka kwa ajali ya mara kwa mara ambapo amesema ajali hizo zimesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 94 kwa ajili ya ukarabati hali inayohatarisha uwezekano wa mradi huo kuwa endelevu.
Akielezea hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaoendelea kukiuka sheria, meneja uhusiano wa DART Bwana William Gatambi amesema Dart kwa kushirikiana na jeshi la polisi, wizara ya mambo ya ndani, Tanroad pamoja na jiji la Dar es Salaam wako katika hatua za mwisho za kutayarisha rasimu ya sheria ndogondongo zitakazo toa adhabu kwa wanaokaidi utaratibu wa matumizi sahihi ya miundombinu hiyo Dart.
Chanzo-ITV
Social Plugin