Wakati leo ni Siku ya Mama Duniani, kijana mmoja wa mjini Musoma,
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi, dada zake
wawili na wanawake wengine wawili jirani wa familia yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema jana kwamba
tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 10 alasiri wakati mama wa
kijana huyo alipofika nyumbani kutoka kazini akiwa na mtoto wake wa kike.
Akisimulia mkasa huo, Ng’anzi alisema baada ya mama huyo kufika nyumbani
na mtoto hao, kijana huyo alimvamia na kumbaka huku rafiki yake (rafiki
wa mbakaji) akilinda mlango wa kutokea ili kuwazuia wasitoke.
“Vijana wengine marafiki wa kijana huyo walikuwa kwenye geti wakilinda
ili kuwazuia walioko ndani wasitoroke,” alisema Kamanda.
Kamanda alisema kijana huyo mbakaji alipomaliza kumtendea mama na dada
zake unyama huo alimwamuru mama yake mzazi kuwapigia simu marafiki zake
ili wafike nyumbani hapo na walipofika kijana wa mama huyo aliwateka
huku akiwatishia kwa panga na kuwabaka kwa kuwaingilia kinyume na maumbile.
Alisema baada ya kumaliza kuwafanyia ukatili huo, aliwapiga picha
wanawake hao wakiwa uchi kwa kutumia simu yake ya mkononi na kisha
kuwaamuru kuondoka katika nyumba hiyo bila kelele.
“Pia aliwatisha kwa kuwaambia wasithubutu kusema popote kitendo
alichowafanyia na endapo watafanya hivyo aliwaambia atawaua,” alisema
Kamanda Ng’anzi
Alisema baada ya kijana huyo na kundi lake kuwaachia wanawake hao
walikimbilia nyumbani za jirani na kutoa taarifa.
Baada ya taarifa hizo, majirani walijikusanya na kwenda kumvamia kijana
huyo wakiwa na silaha za jadi sambamba na kutoa taarifa polisi.
“Polisi walifika eneo la tukio na kuwakuta wananchi wakiwa wamewakamata
vijana hao wawili na tayari walikuwa wamejeruhiwa vibaya, hivyo wapo
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa ajili ya matibabu lakini wakiwa
chini ya ulinzi wa polisi na watafikishwa mahakamani wakati wowote”
alisema Kamanda.
*Mama azungumza*
Akizungumzia tukio hilo, mama mzazi wa kijana huyo huku akibubujikwa na
machozi alirejea kile kilichosemwa na Kamanda Ng’anzi kwamba alibakwa na
kuamuriwa kuwaita kwa simu majirani zake.
Wanawake wengine waliobakwa walisema kitendo walichofanyiwa na kijana
huyo ni cha kinyama, hakivumiliki katika jamii na kwamba walichofanyiwa
ni aibu kusimulia katika vyombo vya habari.
“Mimi nilipigiwa simu na mama yake mzazi kuwa niende kwake mara moja
kuna kitu anataka anieleze, nami nikaenda kuingia sebuleni namkuta yupo
na kijana wake, binti na kijana mwingine, ghafla akaja huyu mwenzangu,
tukashangaa tunaamriwa kwa panga ingieni humu, tukaingia na kuanza
kufanyiwa ukatili,” alisema mama huyo aliyefanyiwa unyama.
*Majirani wamzungumzia mbakaji*
Wakizungumzia tukio hilo, majirani Doto Ochayo na Pendo Elias walisema
kijana huyo ni kibaka mzoefu na kuwa hiyo si mara ya kwanza kumbaka mama
yake. Pia, walisema kwamba alishawahi kufungwa jela miaka 15 na ametoka
hivi karibuni.
*Ukubwa wa tatizo*
Juzi, bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison
Mwakyembe alisema hadi Machi, mashauri ya ubakaji na ulawiti yaliyokuwa
mahakamani ni 2,031 huku takwimu zikionyesha kuwa kila siku watu 19
hubakwa na kulawitiwa.
Hali hiyo ni sawa na watu 570 wanaobakwa au kulawitiwa kwa mwezi au watu
6,840 kwa mwaka.
Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Chama cha Wanahabari Wanawake
Tanzania (Tamwa) inadai kuna ucheleweshaji na upotoshwaji wa ushahidi wa
kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika
ngazi ya Mahakama, polisi na baadhi ya madaktari hospitalini.
Tamwa ilibainisha kuwa jumla ya kesi 62 za ubakaji zimeshindwa kutolewa
hukumu au uamuzi na Mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika
kipindi cha 2014 hadi 2015.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa ni kesi moja tu ambayo mtuhumiwa
alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi 43 bado ziko mahakamani huku
kesi 17 hazijafishwa mahakamani.
Mwanasiasa mkongwe nchini, Anna Abdallah alisema kushamiri kwa matukio
hayo kunachangiwa na kuongezeka kwa kasi mmomonyoko wa maadili nchini.
Alisema katika baadhi ya maeneo, matukio ya ubakaji na ulawiti
yanafanywa na ndugu kwa kusukumwa na imani za kishirikina.

Social Plugin