Mamlaka ya Mapato (TRA) Yataifisha Sukari ya Magendo Mifuko 5319 na Kugawa Bure Kwa Wananchi


Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Million 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.


Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.


Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Million 246.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post