Mbunge Wa Shinyanga Mjini Stephen Masele Awachimba Mkwara Wakandarasi,Tazama Picha Ziara Yake


Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele ameonya wakandarasi wanaojenga miradi ya maendeleo chini ya kiwango jimboni kwake, na kutaka miradi hiyo waijenge kwa hadhi ya juu kulingana na pesa wanazopewa na siyo kuilipua na kuingizia hasara serikali fedha za matengenezo ya mara kwa mara.



Masele ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa jimboni mwake na kukuta mradi mmoja wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Masekelo ambayo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi walimu Sita, kutaka kujengwa chini ya kiwango kutokana na Matofari na kokoto kutokuwa na ubora.


Mheshimiwa Masele amekagaua miradi ya ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa Mawili, Matundu ya vyoo 18 katika shule hiyo ya Masekelo, na ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Tanroad km 2.3 na zile zinazojengwa katikati ya mji Kilomita 13.1 na kuwataka wakandarasi wote kujenga miradi hiyo kwa kiwango kinachotakiwa.


“Mkurugenzi mkandarasi huyu anayetaka kujenga nyumba hii ya walimu chini ya kiwango, kwanza tofari na hizi kokoto aziondoe aweke tofari zingine tena na ujenzi wake asimamiwe kikamilifu maana asije akalipua kazi na hapo baadaye nyumba hii ikaja kuleta maafa”, amesema Mheshimiwa Masele.


“Pia naagiza wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya Maendeleo kwenye jimbo langu waijenge kwa kiwango kinachotakiwa na siyo kulipua kazi ili miradi hii ipate kudumu kwa muda mrefu na kutekeleza miradi mingine ambayo itaondoa kero kwa wananchi na kuufanya mji wa Shinyanga kuwa wa kisasa na kukua kiuchumi”,ameongeza Mheshimiwa Masele


Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna amesema mkandarasi anayejenga nyumba hiyo ya walimu alishamwambia aondoe tofari hizo na kokoto lakini amekuwa mkaidi, huku akibainisha kwa mkandarasi atakaye jenga miradi chini ya kiwango atakuwa amejiondoa kupata kazi tena .

Angalia picha hapa chini ziara ya mheshimiwa Masele leo jimboni kwake

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele akiwa na mkurungezi wa halmshauri ya manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakikagua matundu vya vyoo 18 vilivyomalizika kunjengwa katika shule ya sekondari Masekelo iliyopo katika manispaa hiyo.Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog


Zoezi la kukagua matundu ya vyoo likiendelea

Mheshimiwa Masele akikagua choo

Mheshimiwa Masele (kulia) akiteta jambo na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna

Mheshimiwa Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa sekondari Masekelo


Mheshimiwa Masele na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga wakielekea kwenye eneo panapojengwa nyumba ya walimu

Mheshimiwa Masele akikagua ujenzi wa nyumba ya walimu ambayo itahifadhi walimu sita itakayokamilika mwezi Julai mwaka huu na kughalimu shilingi milioni 150 ambapo ndipo amebaini matofari na kukoto zinazotumika kujenga nyumba hiyo hayana ubora na kuagiza tofari na kukoto ziondolewe ziletwe zenye kiwango bora.

Mheshimiwa Masele akiwa eneo la ujenzi na mhandisi wa ujenzi wa manispaa ya Shinyanga Simon Ngagani

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo

Masele kushoto katikati Mkurugenzi mwisho mhandisi Simon Ngagani (kulia) wakiangalia darasa lililomalizaka kujengwa kwenye shule hiyo ya Masekelo


Mheshimiwa Masele akiwa nje ya darasa hilo
Mheshimiwa Masele akizungumza na wanafunzi wa shule ya Masekelo na kuwataka wasome kwa bidii il iserikali hapo baadae ipate wataalamu wake pamoja na kufanikiwa katika maisha yao na kusaidia wazazi wao.

Mheshimiwa Masele akizungumza na wanafunzi wa shule ya Masekelo na kuwataka wasome kwa bidii il iserikali hapo baadae ipate wataalamu wake pamoja na kufanikiwa katika maisha yao na kusaidia wazazi wao.

Mheshimiwa Masele akiwa katika eneo la miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami km 2.3
Mheshimiwa Masele akikagua miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami km 2.3 huku akitoa Maelekezo ujenzi huo ujengwe kwa kiwango kinacho takiwa ilibarabara hizo zidumu kwa muda mrefu, Kulia kwake ni Paulo Saitabu mshauri wa ujenzi wa barabara hiyo ya Tanroad akipokea Maelekezo hayo ya ujenzi kwa kiwango cha juu.Kushoto ni Godfley Set ambaye ni Msimamizi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya JASCO

Mheshimiwa Masele akitoa maelekezo



Mheshimiwa Masele akikagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zinazojengwa katika kati ya mji wa Shinyanga kwa ufadhili wa Benki ya Dunia zenye urefu kilomita 4.4 na kutarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka huu chini ya Mkandarasi (JASCO) ambaye pia atajenga barabara ya Km 13 katika manispaa hiyo kwa thamani ya shilingi bilioni 15.4



Mbunge Masele akiwa na diwani wa viti maalumu tarafa ya Ibadakuli Zuhura Waziri wakibadilisha mawazo wakati wakikagua Jenzi hizo za barabara kwa kiwango cha lami katikati ya Mji wa Shinyanga.



Masele akiendelea kukagua ujenzi wa barabara

Kushoto ni Godfley Set ambaye ni Msimamizi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya JASCO akitoa maelezo kwa mheshimiwa Masele jinsi ujenzi wa barabara hizo za katikati ya Mji zinavyojengwa na kutarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka huu kwa kiwango cha Lami.


Mheshimiwa Masele akiendelea na zoezi la ukaguzi

Mbunge Masele akisalimiana na wapiga kura wake na kuwaahidi mambo mazuri ikiwa ndiyo amekuja kuanza kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni
Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake

Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake

Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake


Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake

Wapiga kura wakifurahia jambo

Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake

Mheshimiwa Masele akiongea na wananchi

Mbunge Masele akisalimiana na mwananchi
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم