BOB Chacha Wangwe (24), mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii.
Akisoma kesi hiyo namba 167, Paul Kagoshi mbele ya Waliarandwe Rema, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo alisema kuwa, Bob Chacha Wangwe amefikishwa mahakamani hapo kwa kutenda kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake Facebook.
Mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya; “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”
Social Plugin