Baada ya klabu ya Yanga kuhitaji point tatu ili itangazwe kuwa Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania msimu wa 2015/2016 , May 8 2016 ilikuwa siku ya mchezo kati ya Simba dhidi ya Mwadui FC mchezo huu ulikuwa na nafasi ya kumpa Ubingwa Yanga kwa sababu Simba ndio ilikuwa kwenye mbio za kuwania Ubingwa sambamba na Yanga.
Baada ya Azam FC kupoteza point tatu katika mchezo wake wa 156 wa Ligi Kuu waliocheza dhidi ya Mbeya City kwa kumtumia Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano, mpinzani pekee wa Yanga katika mbio za kuwania Ubingwa ilikuwa ni klabu ya Simba, ambayo leo May 8 2016 imekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka Mwadui FC.
Goli la dakika ya 73 la Mwadui FC lililofungwa na Jamal Mnyate lilifanya Simba kukosa matumaini ya kutwaa Ubingwa hata kama watashinda mechi zao tatu zilizobakia na Yanga wakafungwa mechi zote tatu, Yanga hadi sasa wana point 68 wakati Simba wana point 58 hivyo wakishinda mechi zao tatu watakuwa na point 67 bado.
Presha ya mchezo ilikuwa juu kwa wachezaji wa Simba baada ya kufungwa goli na Mwadui FC, kiasi kwamba wachezaji wa Simba waliongeza jitihada za kutafuta goli walau la kusawazisha, lakini mchezaji wao Ibrahim Ajib aliambulia kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika za nyongeza kwa kumchezea rafu Salum Kabunda.
Social Plugin