Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeahirisha shughuli zake za bunge leo majira ya saa tano asubuhi baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) kuomba mwongozo na kutaka sakata la wanafunzi zaidi ya 7000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM waliokwama Dodoma baada ya kufukuzwa chuoni lijadiliwe.
Baada ya Mhe.Nasari kuwasilisha hoja hiyo, naibu spika Dkt.Tulia Ackson Mwansasu, alikataa kujadiliwa kwa hoja hiyo hali iliyosababisha hali ya hewa kuchafuka bungeni.
Kauli ya naibu spika kukataa kujadiliwa kwa hoja hiyo, iliwanyanyua wabunge wa upinzani na baadhi ya wa CCM wakipinga kauli hiyo huku wakiwa wamesimama jambo ambalo lilisababisha kuaihirishwa kwa bunge hadi saa 10:00 jioni huku akiagiza kukutana kwa kamati ya uongozi ya Bunge
Social Plugin