Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameapishwa Rasmi kuwa Rais wa nchi hiyo katika viwanja vya Kololo nchini humo na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Afrika akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka Tanzania.
Haya Ndiyo Yaliyojiri
Amewapongeza raia wa Uganda kwa kupiga kura kwa wingi katika kila sekta ya uongozi.Vilevle amevipongeza vyama vya upinzani kwa kushinda viti mbali mbali.
13.45pm:Rais wa Deby amehutubia kwa lugha ya kifaransa.
13.33pm:Museveni asema ICC ni bodi isiyo na maana.''Tuliunga mkono icc tukidhani ni mahakama nzuri lakini baadaye tukagundua ni mahakama yenye watu wasio na maana''.Museveni ameyasema hayo baada ya kumtambua rais wa Sudan Omar el Bashir
13.23pm:Baadhi ya viongozi waliotambuliwa katika sherhe hiyo ni rais Uhuru Kenyatta wa kenya
Yoweri museveni amkaribisha rais wa Zimbabwe,Omar el bashir wa Sudan.
13.17pm:Miongoni mwa marais wanaohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na rais wa Sudan Omar el Bashir anayeswaka na mahakama ya uhailifu wa kivita katika eneo la Darfur na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
13.13pm:Jeshi la Uhanda latoa heshima zao kwa rais Museveni hivi sasa.
13.09pm:Wimbo wa taifa unaimbwa
12.56pm:Ni wakati ambapo ndege za jeshi zinatoa heshima zao kwa rais Museveni.Ndege hizo zinaonyesha uwezo wake wa kulilinda taifa la Uganda chini ya uongozi wa rais Museveni.
12.38pm:Museveni amekabidhiwa vifaa muhimu vya madaraka ikiwemo katiba,ngao ya mamlaka,bendera na upanga ambao ni ishara ya jeshi.Na sasa ni zamu ya jeshi la taifa hilo kumpatia heshima rais huyo.
12.15pm:Rais Museveni alikagua gwaride la jeshi baada ya kuapishwa rasmi
12.10pm:Rais Yoweri Museveni aapishwa rasmi na jaji mkuu
Baadhi ya watumbuizaji wa hafla hiyo
12.05pm:leo rasmi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko ili watu watokeze kwa wingi kwa sherehe hizo. Ingawaje bado kuna hali ya wasiwasi kwa vile chama cha upinzani na FDC na mgombea urais wa zamani Dk Kizza Besigye bado wanakana ushindi wa Museveni.
12.00pm:Rais Yoweri Museveni kuapishwa kuwa rais kwa muhula wa saba mfululizo nchini Uganda
Museveni kumkabidhi madaraka Museveni si jipya kwa Waganda. nani Rais ambaye alilaumu mwaka 1986, viongozi wa Afrika kukaa madarakani kwa muda mrefu sana.