Aliyesimama ni Mkurugenzi wa kampuni ya Lutandula's Company Ltd Alphonce Magessa akitoa ufafanuzi wa kemikali mpya mbele ya katibu tawala wa wilaya ya Kahama Thabit Ole Matepeti
Ofisi ya madini mkazi wilayani Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kuzunguka katika maeneo ya machimbo ya wachimbaji wadogo ili kutoa elimu ya Matumizi ya Kemikali mpya ya kuchenjulia dhahabu ya Gold Dressing Agent (G.D.A).
Wito huo umetolewa mjini Kahama na Katibu tawala wa wilaya Thabit ole Matepeti aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika Semina ya mafunzo ya matumizi ya Kemikali hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Lutandula’s Company Ltd kwa wadau wa shughuli za madini wilayani Kahama.
Matepeti amesema kuwa wachimbaji wadogo wakipewa elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya Kemikali mpya ya kuchenjulia Dhahabu ya G.D.A itasaidia kuinua vipato vyao,ikiwa ni pamoja na kuokoa afya zao na kulinda mazingira kwa ujumla.
Akielezea umuhimu wa Kemikali hiyo Afisa madini Mkazi wilayani Kahama Sophia Omary amesema kuwa licha ya kukamata dhahabu kwa haraka mabaki ya kemikali hiyo ina uwezo wa kutumiaka kama mbolea tofauti na kemikali zingine.
Kwa upande wake Afisa kutoka ofisi ya mkemia wa Serikali kanda ya ziwa Rwige Ogunya amesema kuwa Kemikali ya G.D.A haina madhara kama zilivyo kemikali ya Mercury na Cyanide ambazo mara nyingi zimetajwa kusababisha madhara kwa binadamu,wanyama na mazingira.
Naye mkurugenzi wa Kampuni ya Lutandula’s Companya Ltd ambaye ndiye Msambazaji wa kemikali hiyo barani Africa Alphonce Magessa amesema kuwa kemikali hiyo itasaidia kuinua uchumi wa wachimbaji wadogo kutokana na uwezo wake wa kukamata dhahabu na kuiiacha ikiwa na ubora wake asilia.
Sambamba na hayo Magessa ameongeza kuwa Lengo la kuingiza kemikali hiyo nchini na barani Africa kwa ujumla ni kulinda usalama wa wafanyakazi migodini pamoja na viumbe hai vinavyozunguka maeneo ya migodi.
Awali akielezea ubora wa kemikali hiyo Mshauri Mkuu wa kampuni ya Lutandula’s Baraka Adroph amesema kuwa Kemikali hiyo aina viambata vyenye madhara hali unayoweza kukaa nayo ndani na kuendelea na shughuli zozote zile pasipo kuleta madhara.
Kemikali mpya ya Uchenjuaji Madini ya Gold Dressing Agent (G.D.A) inayopataikana barani Africa kwa sasa inapatikana wilayani Kahama kupitia kampuni ya Lutandula’s Company Ltd.
Kwa yeyote anayehitaji Kemikali hii au anahitaji kujua mengi kuhusu Kemikali hii Mpya wasiliana na Mkurugenzi Kwa namba +255 765 245 514 au +255 28 2711111 au E-mail alphonce.magesa@lutcol.co.tz au Bofya hapa kwa maelezo Zaidi http://lutcol.co.tz/
MATUKIO KATIKA PICHA
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Lutandula's Company Ltd wakiwa
katika semina ya kutambulisha kemikali hiyo kwa wadau wa madini.
Baadhi ya wanafunzi waliohitimu mafunzo ya madini katika vyuo vya
madini vya Dodoma na Shinyanga wakiwa katika semina ya kutambulisha kemikali
mpya ya Gold Dressing Agent (G.D.A)
Baadhi ya wadau wa masuala ya madini wakiwa katika semina hiyo,wa
kwanza kushoto ni mgeni kutoka nchini China ambako kemikali hiyo inatengenezwa.
Mkurugenzi wa kampuni ya Lutandula's ,Magessa akitoa maelezo namna
alivyoanza kuagiza kemikali hiyo.
Wadau wa kampuni ya Lutandula's wakiwa katika semina hiyo.
Meneja ufundi wa kampuni ya Lutandula's company Ltd, Idrisa
Mafumbi akifafanua jambo katika semina hiyo.
Mtaalamu wa masuala ya utunzaji kemikali kutoka kampuni ya
Lutandula's Amani Magessa akijitambulisha mbele ya wana semina.
Mhasibu wa Kampuni Lutandula's Company Ltd Remmyfrida Mswahili akijitambulisha
katika semina hiyo
Injinia wa madini wa Kampuni ya Lutandula's Company Ltd Frolian Mutta
akifafanua jambo katika semina yamafunzo ya matumizi ya kemikali mpya ya Gold
Dressing Agent.
Mmoja wa wanafunzi waliohitimu katika Chuo Cha Madini Dodoma akiuliza
swali ya namna kemikali ya Gold Dressing Agent (G.D.A) inavyofanya kazi.
Afisa Madini Mkazi kutoka wilaya ya Kahama Sophia Omary akielezea
umuhimu wa kemikali hiyo na mipango ya ofisi yake katika kuwafikia wachimbaji
wadogo na kuwapa elimu hiyo.
Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Lutandula's Baraka Adroph akielezea
namna kemikiali ya G.D.A inavyotofautiana na kemikali nyingine.
Baraka Adroph akiendelea na ufafanzi wa kemikali hiyo.
Katibu tawala wa wilaya ya Kahama Thabit Ole Matepet akimpa mkono
wa hongera mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Lutandula's Company Ltd , Philipo
Magessa baada ya kufungua semina hiyo.
Afisa kutoka ofisi ya Mkemia Kanda ya ziwa , Rwige Ogunya akitoa
elimu kwa wana semina katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA KIJUKUU BLOG