Polisi Kigoma Wamshikilia Mtu Anayedaiwa kuwa ni Jambazi, Wanasa Wahamiaji Haramu 30

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji  anayesadikika kuwa jambazi kwa kukutwa na risasi tisa za zunduki aina ya SMG.


Jeshi hilo pia linawashikilia wahamiaji haramu 30 kutoka katika nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jana, kamanda Wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma SACP,Frednand Mtui alisema Askari polisi wakiwa doria walifanikiwa kukamata wahamiaji haramu na kupatikana silaha hizo.

Mtui alisema mnamo tarehe 30,Aprili mwaka huu,  askari polisi walifika nyumbani kwa Hamza Hassan,(56) Mkazi wa Buzebazeba Wilayani Kigoma mtuhumiwa alikamatwa baada ya kukutwa na silaha hizo chumbani kwake.


Alisema mtuhumiwa huyo anashtumiwa kwa tuhuma za kujihusisha na ujambazi, kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria na Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za Kisheria pindi uchunguzi utakapo kamilika.


"Jeshi la polisi Mkoani Kigoma linawajulisha Wananchi kuwa hali ya ulinzi na Usalama ni shwari hata hivyo kumekuwepo na matukio baadhi ambayo tumeweza kuyatatua",alisema Mtui.


Hata hivyo katika msako ulioendelea kufanyika katika wilaya zote  wiki hii jeshi la polisi lilikamata wahamiaji haramu 30,pombe ya moshi lita 80 na bangi kilo moja na nusu.



Mtui aliwaomba wananchi wa Mkoa huo kuendelea kutoa taarifa dhidi ya uharifu kwa jeshi hilo na kwa wasiwapokee wahamiaji wanaoingia bila vibali hali inayoweza kupelekea uhalifu mkubwa.
⁠⁠⁠Na Rhoda Ezekiel -Malunde1 blog Kigoma,

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post