
Akizungumza na vyombo vya habari leo Snura amesema wakati wa utayarishaji wa video hiyo mvua ilinyesha hivyo madansa walilowana.
"Baada ya kuona wamelowa ilibidi tusitishe kupeleka katika televisheni na kuiacha you tube, Snura hajafungiwa bali video yangu ilisitishwa na mimi nilizuiwa kujihusisha na sanaa mpaka nijisajili," amesema Snura.
Meneja wa mwanamuziki huyo Hemedi Kavu amesema tayari walishakwenda Basata tangu jana kuomba usajili, leo wamepatiwa cheti cha usajili.
"Tumeshajisajili Basata, pia tayari tumeshaitoa video hiyo kwenye mtandao wa YouTube, tumeshalitekeleza na akaunti ya wimbo huo imeshafutwa na tunatarajia kuifanya video hiyo upya," amesema Hemedi Kavu.

Social Plugin