SUMATRA Yatangaza Nauli Za Usafiri Wa Mabasi Yaendayo Haraka,Angalia Hapa


Hatimaye Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi kuwa ni 400, 650 na 800 kwa safari za Mbezi mwisho hadi Kivukoni.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya Kimara kwenda Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo - Kivukoni.


Amesema nauli ya Sh800 ni Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.


“Chombo chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara zao” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu nauli zitakazotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.

Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu viwango vipya vya nauli baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya nauli iliyopendekezwa awali na Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe (Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald Lwakatare wakimkabidhi leseni ya usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Katikati)

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe baada ya kupokea leseni ya usafirishaji kutoka SUMATRA.

PICHA NA FATMA SALUM

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post