Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TFF Imetangaza Mchezaji Bora Mwezi Mei 2016,Atapokea Zawadi ya Milioni 1


Shirikisho la soka Tanzania TFF leo Mei 30 2016 kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter na tovuti rasmi ya shirikisho hilo, wamemtangaza mshambuliaji wa JKT Ruvu Abdulrahman Musa kuwa ndio mchezaji bora wa mwezi Mei wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2017.

Abdulrahman Musa amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi kwa kuwazidi mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe anayeichezea Yanga Donald Ngoma na mchezaji wa Mgambo Shooting ya Tanga Ali Nassoro, Musa katika mzunguuko wa mwezi May alicheza mechi tatu na kufanikiwa kufunga magoli manne.

Musa atazawadiwa milioni 1 ya kitanzania kufuatia ushindi huo, kama utakuwa unakumbuka hawa ni mastaa wengine waliotwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi msimu wa 2015/2016 Hamisi Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam (Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com