Ni siku mbili zimepita toka tushuhudia ile fainali ya michuano ya klabu Bingwa Ulaya kwa mwaka 2016, fainali ambayo ilichezwa katika uwanja wa San Siro Milan Italia, hiyo ilikuwa fainali inayozihusisha timu kutoka nchi na jiji moja Hispania Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid.
Leo Mei 30, 2016 shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 18 kutoka timu mbalimbali barani Ulaya na kuwataja kama ndio wachezaji waliofanikiwa kuunda kikosi bora cha msimu wa 2015/2016 kwa UEFA, list ya wachezaji hao waliotajwa hakuna hata jina la mchezaji yoyote kutoka Ligi Kuu Uingereza.
Ni vilabu vitano tu ndio vimefanikiwa wachezaji wake kutajwa katika list ya wachezaji 18 wa UEFA kwa msimu wa 2015/2016, Atletico Madrid na Real Madrid zimetoa wachezaji sita sita, wakati FC Barcelona imetoa wachezaji watatu, FC Bayern Munich imetoa wachezaji wawili na Paris Saint Germain imetoa mchezaji mmoja.
Social Plugin