Vyombo
vya habari vya asilia hususani magazeti vinakufa. Hivi sasa vyombo
hivyo vinajikongoja kutokana na mauzo hafifu na mdororo wa mapato
kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi.
Ila
wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi
mtandaoni humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa
Pew Research Centre unaeleza.
Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the News Media 2015,”)
imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media),
Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu.
Utafiti
huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni
wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo
gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala
zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni
Hivi
sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko.
Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao
kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza
kutishia amani ya magazeti.
Upande
wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza
kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao,
maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti.
Upande
wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi
anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini
wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya
tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio
magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
“Ni
kweli kwamba Tanzania bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha
habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si
uongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati
muda si mrefu print media itakwenda na maji”, amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.