Wabunge wanawake wa Upinzani wametoka wote nje ya Bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga (CCM ) aliyedai jana kuwa viti maalum Ukawa hutolewa kwa rushwa ya ngono.
Mlinga alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia hotuba Wizara ya Katiba na Sheria ambapo alisema ili uweze kuwa mbunge wa viti maalum chadema, lazima ufanye mapenzi na kiongozi wako wa chama.
Wabunge hao leo asubuhi waliomba mwongozo kwa Naibu Spika kupitia kwa Mbunge Sophia Mwakagenda wa viti maalumu (Chadema) kumtaka mbunge huyo athibtishe kauli yake lakini hawakusikilizwa na badala yake Naibu spika aliwataka wakae chini.
Baada ya mabishano ya dakika kadhaa pasi kusikilizwa, wabunge hao walisimama wote na kuamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa.
==>Msikilize hapa Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge hao kutoka nje