JESHI la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu 30 waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya kuwabaka wanawake wajane na waseja katika maeneo ambayo hayana ulinzi wa kutosha katika mitaa ya Vamia na Katubuka mkoani Kigoma.
Akizungumza na Waandishi wa habari kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma SACP ,Fredinand Mtui amesema kutokana na wimbi la uhalifu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji la baadhi ya vijana kuwaingilia kimwili kinamama na mabinti bila ridhaa yao maaarufu kama TEREZA limedhibitiwa baada ya msako.
Amesema askari polisi walifanya msako katika maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakilalamikia vitendo hivyo ambayo ni Vamia na Katubuka na kufanikiwa kuwakamata vijana 30 na upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini wahusika wengine waweze kufikishwa mahakamani.
Mtui amesema katika ukaguzi uliofanywa na jeshi la polisi ulibaini mambo yanayoweza kusababisha vitendo hivyo ni mitaa hiyo ni giza na hakuna taa za nje ,milango ya ndani sio imara na haina komeo za ndani pia ushirikiano baina ya majirani ni mdogo.
Pia katika mitaa hiyo wazururaji ni wengi hasa nyakati za usiku na na maeneo yamezungukwa na virabu vya pombe za kienyeji ambavyo havifungwi kwa muda uliopangwa ambapo vijana wengi waishio katika maeneo hayo hutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ijulikanayo kwa jina la BUNGA hali inayosababisha kutokea kwa matukio hayo.
“Jeshi la polisi limeimalisha doria katika maeneo hayo ilikudhibiti uharifu huo pia nitoe wito kwa Wananchi kwa wananchi kulekebisha milango yao iwe imara,kujenga ushirikiano baina ya majirani iliwaweze kudhibiti uhalifu unapo tokea na sheria na kanuni za za uzaaji pombe zifuatwe”,amesema mtui.
Hata hivyo kamanda amewataka vijana wenye tabia ya kutembea usiku waziache,na kwa atakayekamatwa anatembea kuanzia saa sita usiku atakamatwa na kufikishwa polisi.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano pindi wanapobaini kuna vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza katika mitaa yao.
Na Rhoda Ezekiel-Malunde1 blog Kigoma
Social Plugin