Angalia Picha 35!! SUMATRA Yakutana na Wadau wa Sekta ya Usafiri Wa Barabara Mkoa wa Shinyanga



Hapa ni katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za serikali mkoa wa Shinyanga ambapo leo kumefanyika semina/warsha ya siku moja ya Utoaji elimu kuhusu sekta zinazozibitiwa na mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).Warsha hiyo imekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri kwa njia ya barabara katika mkoa wa Shinyanga wakiwemo madiwani,mahakimu,mawakili wa serikali,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani,maafisa kutoka mamlaka ya Mapato ,waandishi wa habari na maafisa kutoka SUMATRA wakiongozwa na Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki aliyemwakilisha mkurugenzi mkuu wa SUMATRA Gilliard Ngewe.


Mgeni rasmi alikuwa Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.

Akizungumza katika warsha hiyo Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki aliwataka wadau wa usalama barabarani kuwa na ushirikiano wa hali ya juu ili kukabiliana na changamoto za sekta ya usafiri kwa njia ya barabara.

Mutaki alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na miundombinu isiyo rafiki kwa usafirishaji,baadhi ya vyombo vya usafirishaji kukosa ubora,ukiukwaji wa sheria,kanuni za usalama barabarani.

Mutaki alisema ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya usafiri kwa njia ya barabara kunahitajika ushirikiano wa hali ya juu kwa taasisi na serikali kwa ujumla kwani jukumu likiachwa SUMATRA pekee lengo la kuboresha usafiri kwa wananchi haliwezi kufanikiwa.

“SUMATRA imeona umuhimu wa ushirikiano wa wadau na ndiyo maana tunakutana nao ili kupata uelewa wa sheria,kanuni na masharti mbalimbali ya usafirishaji kwa njia ya barabara,tunawaomba waendeshaji wa vyombo vya moto ili kupunguza changamoto za barabarani ili kupunguza ajali”,aliongeza Mutaki.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo katika warsha hiyo,ametuletea picha zaidi ya 30 tazama hapa chini

Aliyesimama ni Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki akizungumza katika warsha hiyo ambapo alisema maeneo yanayothibitiwa na SUMATRA kuwa ni usafiri wa barabara,usafiri wa reli,hudumaza bandari na meli na ulinzi na usalama wa majini

Wajumbe wa warsha hiyo wakiwa ukumbini
Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki akielezea sheria na kanuni zinazotumiwa na SUMATRA

Warsha inaendelea

Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa Shinyanga Chacha Maro
Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki akisisitiza jambo katika warsha hiyo

Warsha inaendelea
Warsha inaendelea

Aliyesimama ni mgeni rasmi ambaye ni Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza katika warsha hiyo ambapo alisema changamoto nyingi za usafiri wa njia ya barabara zinatokana na watu kutojua sheria,taratibu na kanuni za usalama barabarani matokeo yake wadau kutupiana lawama.
Msovela alisema makosa mengi ya usalama barabarani yanatokana na ulegevu katika usimamizi wa sheria huku akiomba elimu iendelee kutolewa kwa waendesha bodaboda,magari na waendesha baiskeli kwani ajali nyingi zinatokana na uzembe.
Kushoto ni Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki akiwa na afisa mfawidhi SUMATRA mkoa wa Shinyanga Bahati Musiba

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza katika warsha hiyo

Warsha inaendelea kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa Shinyanga Chacha Maro

Warsha inaendelea

Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Askari wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Askari wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Askari wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga wakichukua kumbukumbu muhimu katika warsha hiyo

Madiwani wa manispaa ya Shinyanga Hassan Mwendapole na Shela Mshandete wakiwa ukumbini

Warsha inaendelea

Wawakilishi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini

Warsha inaendelea
 
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akizungumza katika warsha hiyo

Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini....

Maafisa kutoka SUMATRA wakiwa ukumbini

Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki akiwasilisha mada katika warsha hiyo
 
Afisa Sheria Mkuu Kutoka SUMATRA Leticia Mutaki akiwasilisha mada

Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
 
Afisa leseni na udhibiti makao makuu SUMATRA Mohamed Zander akitoa mada ya utambuzi wa makosa wakati wa ukaguzi wa leseni barabarani
 
Warsha inaendelea... kushoto ni afisa leseni na udhibiti makao makuu SUMATRA Mohamed Zander akiwa na afisa mfawidhi SUMATRA Bahati Musiba (kulia)

Wajumbe wa warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
 
Picha ya pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri kwa njia ya barabara katika mkoa wa Shinyanga

Picha ya pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri kwa njia ya barabara katika mkoa wa Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post