Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha!! Msafara wa Mazishi ya Bondia Maarufu Muhammad Ali

 
Makumi ya maelfu ya watu wamemuaga aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali nyumbani kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.

19.27pm:Bondia wa Uingereza Amir Khan ambaye alikutana na Muhammed Ali mara mbili anasema kuwa Ali alikuwa kielelezo chake.Ali alikuwa na pande nyingi lakini unapoangalia mafanikio yake katika ndondi kwa kweli ni makubwa mno,alisema.

19.18pm:Watu wamejipanga kandokanzo ya barabara huku msafara wa gari lililobeba mwili wa Ali ukiendelea kupita katika maeneo muhimu ya Ali wakati wa maisha yake huku baadhi ya mashabiki wake wakimsifu Ali! Ali !

19.16pm: Ibada ya mazishi itafanyka huko katika uwanja wa michezo wa Louisville

19.04pm:Muhammad Ali alikuwa hanunuliki,hauziki wale kutishwa.Ni msimamo wake ndio uliomleta karibu na wanaharakati wa haki za kibinaadamu nchini Marekani.

18.32pm:Kushindwa kwa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan kuhudhuria mazishi ya Muhammad Ali licha ya kufunga safari nchini Marekani kuhudhuria kumeangaziwa na magaeti mengi ya Uturuki.

18.30pm:Kwa sasa msafara umefika katika eneo la Boulevard
Maelfu wamejipanga barabarani ili kumuaga bondia Maarufu Muhammad Ali wakati msafara ukipita kuelekea mji wa kwao Louisville, Kentucky ambapo leo June 10 2016 anatarajiwa kuzikwa huko. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com