Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Binti Afikishwa Mahakamani Kwa Kutoa Lugha ya Vitisho Kwa Njia ya Simu,Alimtishia Kumuua au Kumroga Mwenzie


Mkazi wa Kijiji cha Misasi Mariamu Nestory (20) amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kujibu shtaka la kutoa lugha ya vitisho kwa njia ya simu.


Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Doroth Mgenyi alidai kuwa Mei 2 saa 8:15 mchana, mshtakiwa huyo kwa kutumia simu aliandika ujumbe wa vitisho kwa Diana Kabula kinyume cha sheria ya makosa ya mtandao kifungu 18 (1) ya mwaka 2015.


Alinukuu ujumbe huyo akidai: “Ujiandae siku utakayoingia anga zangu, sali sala ya mwisho, ulisikia kisa cha Sengerema ndivyo nitakavyokufanya... ikishindikana kukuua kwa mikono yangu nitakuroga uwe kichaa.”


Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana shtaka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com