Jeshi la Polisi Shinyanga Lazuia Ndoa ya Mtoto wa Darasa la Sita,Alikuwa Anaolewa Kwa Ng'ombe 14




Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na shirika la Agape linalopambana na uvunjifu wa haki za watoto wa kike limefanikiwa kuzuia ndoa ya mtoto wa darasa la sita aliyekuwa anaolewa na mwanaume wa miaka 26 kwa mahali ya ng’ombe 14.



Mwandishi wa habari hizi alifika katika kijiji cha Mwigumbi kata ya Maganzo wilayani Kishapu na kukutana na sakata hilo ambapo punde tu baada ya polisi kuvamia eneo hilo wazazi wa watoto hao walikimbia na kujificha pasipojulikana.
Kufuatia hali hali hiyo ndipo polisi walipowakamata vijana hao na kuwafikisha katika kituo cha polisi cha Maganzo ambapo Msaidizi wa Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga Greyfton Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. 


Aidha baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walioshuhudia tukio hilo wametoa maoni yao na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali wahusika ili iwe fundisho kwa watu wenye tamaa ya kupata mali kwa kuozesha watoto wadogo. 

Mkurugenzi wa shirika la Agape John Myola linalohusika na uetetezi wa haki za watoto amesema ndoa na mimba za umri mdogo zinachangiwa na baadhi ya viongozi wa kata na vijiji kushindwa kutambua wajibu wao katika jamii.
 Mkuu wa wilaya ya Kishapu Bi. Hawa Ng’humbi ameagiza watendaji hao pamoja na wazazi wanaohusika kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kusheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post