Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Kada wa CHADEMA Ole Medeye Ahamia UDP Kisa Wabunge wa Upinzani Kutomheshimu Naibu Spika


Kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza leo rasmi kuhamia chama cha UDP.


Ole Medeye amezungumza hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho,Mwananyamala jijini Dar.


Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,pichani katikati ni Mwenyekiti wa chama cha UDP,Mh.John Cheyo akishuhudia tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com